Administration
MUUNDO NA UTAWALA
Mwenyekiti
Kutakuwa na Mwenyekiti ambaye majukumu yake ni:
i. Kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika
ii. Kuitisha na kuongoza mikutano yote ya shirika
iii. Kuwa msemaji wa shirika kwa Mashirika mengine na mialiko ya nje.
iv. Kutafuta mshirika wa nje ambaye atasaidia shirika katika masuala ya fedha, ufadhili, utangazaji na mali ili kutimiza malengo ya shirika.
v. Kuwa msimamizi wa watendaji wote wa ofisi, wakati mwingine kuwaita wakati wowote inapohitajika, pia kuachishwa kazi kwa kupewa endelea na Bodi na Mkutano Mkuu.
vi. Kuwa mwangalizi wa majukumu/shughuli zote za Shirika.
Katibu
Kutakuwa na Katibu ambaye kazi zake ni:
i. Kuwa msimamizi wa shughuli za kila siku.
ii. Kuwa Katibu wa mikutano yote inayofanywa na shirika
iii. Kutayarisha ajenda za mikutano yote inayofanywa na shirika
iv. Kuwa mlinzi wa hati zote za shirika
v. Kufanya shughuli za kupanga hasa ratiba ya mikutano.
vi. Kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na Mwenyekiti.
Mweka Hazina
Kutakuwa na Mweka Hazina ambaye kazi zake ni:
i. Kuwa mwangalizi wa hati za kifedha
ii. Kuandika vitabu vyote vya hesabu hasa marejesho ya mwezi, taarifa ya mapato na matumizi, hesabu za fedha na kuwasilisha kwenye Bodi.
iii. iii. Kupokea fedha na kuweka kwenye Akaunti ya Benki ya Shirika.
iv. iv. Kuwasilisha vitabu vya hesabu na akaunti ya mwisho kwenye Mkutano Mkuu.
v. Kuweka vitabu tayari kwa ukaguzi wa mkaguzi na mjumbe mwingine yeyote pale mahitaji yanapotokea
vi. Kufanya mpango wa fedha wa muda mrefu wa bajeti pamoja na kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya kila robo mwaka kwa Bodi.
vii. Kufanya shughuli zozote za kifedha kama inavyotakiwa na mwenyekiti.
Comments
Post a Comment